Watu kumi na tatu wameripotiwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kufuatia mji huo kukumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizoanza kunyeesha toka siku ya Jumatatu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mkuu wa mkoa wa DSM Mecky Sadick amesema kuwa mpaka sasa watu waliodhibitishwa kufa ni kumi na tatu na zoezi la uokoaji linaendelea.
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam ikiwemo eneo la Jangwani ambalo karibu lote lilifunikwa na maji, maeneo ya Tabata na kigogo ambayo kwa pamoja yote yalikuwa katika hali mbaya kutokana na maji kujaa.
Kiongozi huyo ameongeza maeneo mengi ambayo yamefurika maji kumesababishwa na wananchi katika maeneo hayo kujenga nyumba katika maeneo ambayo hayaruhusiwi na kuziba mifereji iliyokuwa inapitisha maji.
Hapo jana waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka alilazimika kukatisha ziara yake nchini Uganda na kuetmbelea maeneo yaliyoathirika na pia kuanza kutekeleza agizo la rais la kuwataka wananchi wanaosihi mabondeni kuhama mara moja.
rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete alituma salamu za rambirambi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao wameathirika na mafuriko hayo na kuwakata wananchi wanye nyumba kwenye maeneo ya mabondeni kuhama mara moja.
Mvua hizo ambazo zimeendelea kuleta madhara makubwa nchi nzima, zimesababisha miundo mbinu mingi kuharibika ikiwemo madaraja, barabara, reli na nguzi za umeme na kusababisha baadhi ya maeneo kutofikika kirahisi.
Nae mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya Hewa Daktari Agnes Kijazi amesema kuwa eneo la nyanda za juu kusini linalojumuisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Sumbawanga na kanda ya kati maeneo ya Dodoma, Singida na mikoa ya Kigoma na Tabora nayp yanatarajiwa kuwa na mvua kubwa na hivyo kutoa tahadhari kwa wananchi.

No comments:
Post a Comment